IFAHAMU SOYA/ SOY NA FAIDA ZAKE KIAFYA
+255719197319
Sishangai unaweza ukawa hulijui kabisa hili zao. Lakini limeonekana kuwa kama ni zao la maajabu kutokana na linavyofanya kazi na kutatua matatizo kadha wa kadha katika mwili wa binadamu.
Tafiti nyingi zimeonyesha juu ya umuhimu wa soya katika mwili, huku mwili wa mwanamke ukimulikwa zaidi.
Soya huwa na muunganiko wa vitu ambavyo hufanana na estrogen ambacho ni kichocheo muhimu katika mwili wa mwanamke.
Soya ina vitu kama homoni viitwavyo isoflavones( genisein na daidzein)
Vyote hivyo vina umuhimu sana katika mwili wa mwanamke.
Tafiti zinaonyesha kwamba wanawake waishio barani Asia ambako kuna upatikanaji wa hili zao, huepuka matatizo mengi sana kiafya ukilinganisha na wale waishio pale upatikanaji wa hili zao ni mdogo.
Kiafya, soya yenye isoflavones hutatua matatizo yatokanayo na vichocheo ( hormone related disorders)
~Saratani ya titi
~Uvimbe katika mfuko wa mimba
~kuwa na hedhi isiyoeleweka ama inayochukua muda mrefu.
Lakini si kwa wanawake tu, pia kwa wanaume imeonekana kuwa na kazi muhimu kiafya juu ya matatizo yatokanayo na vichocheo.
Pia fahamu kazi kuu za soya katika mwili.
1.Inamkinga mwanamke aliyefikia ukomo wa hedhi kupata kansa ya titi.
Genistein katika soya huzuia protein iitwayo tyrosine kinase, hiki ni kimeng'enya (enzyme) ambacho huchochea ukuaji wa seli za saratani.
Kaa ukijua kwamba mwanamke aliyekaribia ama yuko kwenye ukomo wa hedhi huwa yuko hatarini kupatwa na saratani ikiwemo ya titi.
2. Inaondoa dalili za ukomo wa hedh, kama damu kutoka kwa wingi, vichomi, maumivu makali n.k
3.Inakinga juu ya magonjwa ya moyo.
Hii ni kwa sababu, huondoa mafuta mabaya mwilini(lower density lipoproteins) na huongeza mafuta mazuri ( high density lipoproteins).
Pia huzuia kuvunjwa vunjwa kwa LDH ambayo inaweza kuziba mishipa ya ateri.
4. Huzuia tezi dume.
Hili ni tatizo linalotokana na umri ambapo ni dhahiri huwa kuna upungufu wa homoni unaosababisha prostate ikue kuliko kawaida.
5.Matatizo katika pingili za mgongo hasa sehemu ya kiuno, ambapo mwanamke huwa na maumivu yasiyo na kikomo, hivyo soya ni suluhisho.
6. Huondoa mafuta mabaya katika mwili, inapunguza uzee na kuimarisha nyama za ukeni.
7.Huongeza hamu ya tendo la ndoa
8.Pia ina mchango katika kuzuia magonjwa ya figo, kusaidia mmeng'enyo wa sukari aina ya lactose, galactose, kwa walio na galactosemia.
Kutokana na mazingira yetu imekuwa ni changamoto katika kupata zao hili.
Kuna wengine tayari wana hayo matatizo, hawa hawawezi kupata kiasi kinachotakiwa kwa kula soya yenyewe kama sehemu ya chakula.
Kwa kujali afya yako unaitumia kama kinga pia ukiwa na matatizo ama dalili nilizozitaja hapo juu.
Pia juu ya ushauri kuhusu afya na tibalishe
0 Maoni