*MHIMU SANA KWA AJILI YA AFYA YAKO!!!!*
Soma mpaka mwisho kwa manufaa yako binafsi⤵
Asilimia 80% ya magonjwa huanzia tumboni. Ndio maana tunashauriwa kujali sana tukiingizacho tumboni (milo tunayakula).
Moja ya dalili za kukuonesha kwamba tumboni kumeanza kua na kasoro, ni vile utoavyo haja kubwa, dalili zingine ni tumbo kutoa miungurumo ya kusika hata kwa mtu jirani uliekaa nae!!!
Tukijikita kwenye vile utoavyo choo, yajue haya⤵
Kama unatoa haja kubwa (choo) ya kukatikakatika kama choo cha mbuzi, choo kigumu, choo ambacho kinanata sana kwenye sinki (hakitoki kirahisi), choo cha kuharisha, au kukosa choo kabisa, usipotezee hali hiyo kama hali ya kawaida.
Badala yake, tafuta vyakula vyenye fibers (nyuzi nyuzi), vinasaidia kusafisha mfumo wa chakula.
Vyakula hivyo ni pamoja na;
~Bamia
~Papai na matunda mengine kama chungwa
~Viazi vitamu vya kuchemsha
~Kabichi na mbogamboga zingine
Lakini pia kunywa maji kwa wingi.
Kama una shida hiyo ya choo kisichoeleweka na unaona kawaida tu, kula vyakula hivo mfululizo kwa mda wa wiki 1, utaona mabidiliko na usipoona mabadiliko, basi unahitaji matibabu zaidi kwa sababu shida ni kubwa na inaendelea kukua kimya kimya.
*Sifa za choo unachopaswa kupata;*
●Kisiwe kigumu wala kilaini sana kama cha kuharisha
●Kisiwe cha kunata sana kwenye sinki
●Kisiwe cheupe, kiwe cha kijani kijani.
●Kisiwe cha kukatikakatika kama cha mbuzi
●Kikitoka kiwe kirefu bila ya kukatikakatika usawa wa urefu wa kiganja chako cha mkono
●Harufu yake isiwe ya kunuka sana hadi unapata shida ukiwa chooni
●Kiwe cha moto na chenye kutoa moshi fulani ivi (rahisi kuonekana asubuhi)
●Kama una kula kila siku, basi pata choo kila siku na wakati mwingine mara 1 hadi 3 kwa siku
Zoezi hili ni rahisi kuweza kujichunguza ndani ya siku 3 na kujua kasoro.
Chakula ni dawa, jali sana ulacho kwa sababu ni muhimu sana kwa afya yako.
Ukigundua choo chako kina sifa za hapo juu, upo vizuri hamna shida kwenye mfumo wako wa mmeng'enyo wa chakula, endelea kula vizuri na kunywa maji mengi.
Ukigundua kasoro, kula vyakula nilivyoeleza hapo juu, kunywa maji mengi alafu tofautisha kadri ulivoona kasoro na baada ya wiki nzima ukila vyakula hivyo.
Usipoona tofauti, unahitaji tiba. Usichukulie poa!!!!
Chakula ulichokula, kinasagwa na kumeng'enywa na virutubisho vinavyopatikana, hufyonzwa kupitia ukuta wa mfumo wa chakula (kuanzia mdomoni hadi kwenye njia ya haja kubwa) na kuingia kwenye mirija ya damu ambapo, kiasi cha sukari, vitamini, madini, glycerol, vijenzi protini na mafuta mhimu husafirishwa kupitia mishipa hiyo ya damu hadi kwenye ini ambapo virutubisho hivyo hutunzwa ili kutolewa baadae mwili unapovihitaji.
Mabaki ya mmeng'enyo wa chakula ndio hutolewa kama takamwili (choo).
Homoni toka kwenye kongosho na zingine kwenye mfumo wa chakula, ndizo hutoa taarifa kwenye ubongo ili kukufahamisha kama una njaa tena au bado umeshiba!!!!
Mfumo wa lymph (Lymphatic system) ambao hubeba kinga ya mwili yaani chembechembe hai nyeupe za damu, hubeba baadhi ya mahitaji ya seli hizo nyeupe toka kwenye virutubisho vilivopatikana kwa ajili ya kuimarisha seli hizo na ulinzi (kinga) asilia ya mwili.
Na virutubisho vilivyotunzwa kwenye ini pamoja na seli zingine, ndivyo baadae hutolewa na kutumika na mwili kwa ajili ya kuzalisha nguvu, kiasi cha virutubisho vilivyopelea pamoja na kurekebisha seli zilizolegea au kuziba pengo la seli zilizokufa.
Sasa, mchakato mzima huo unategemea mfumo wa usafrishaji taarifa mwilini ambao pia hutegemea madini na virutubishi vingine tunavyopata kwenye chakula tulacho.
Mfano madini kama ya Kalsiamu, husaidia katika mfumo wa usafrishaji taarifa mwilini, afya ya maungio na mifupa na kuimarisha mfumo wa uzazi wa mwanamke.
Wakati vitamini D, husaidia madini hayo kufyonzwa toka kwenye mfumo wa chakula kulingana na chakula ulichokula kama kina madini hayo.
Madini ya Zinc husaidia kutengeneza chembechembe za rangi nyekundu ya damu, kulinda tezi dume, kuimarisha mfumo wa uzazi kwa mwanaume.
Sasa kama unakula chakula kisichohitajika na mwili, utaendelea kuulundikizia mwili vitu ambavyo hautaki kutunza na mwisho wa siku changamoto nyingi za kiafya huanzia hapo.
Mfumo wa damu ukibalika ovyo utazaa shida za moyo na presha. Hii ni kadhalika pia kama mwili utarundika mafuta mabaya yasiyohitajika mwilini.
Hali hiyo itapelekea shida kwenye mfumo wa usafirishaji taarifa mwilini, hivyo viungo vingine kukosa taarifa na virutubisho vinavyohitajika na hatimae kudhoofu kwa utendaji kazi wa viungo hivyo.
Mwili ukijirundikia sukari mwilini na nyingine kushindwa kubadilishwa kua glycogen (glycogen ni glucose/sukari iliyobadilishwa kua katika mfumo ambao itatolewa ili kutumika baadae), changamoto za kisukari aina ya 2 huanzia hapo.
Madini ya Kalsiamu na Zinc na mfumo wa taarifa ukidhoofu, changamoto kama za uke mkavu, upungufu wa nguvu za kiume na changamoto za uzazi huanzia hapo.
Hivyo, unapotumia dawa kutibu tatizo fulani, usitake matokeo ya haraka labda ndani ya mwezi mmoja shida iwe imeisha wakati hujui ilichukua mda gani ilichukua mifumo ndani ya mwili kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri.
Kupona ni mchakato, kula vizuri na tumia tiba ulizoshauriwa kutumia kurejesha sawa mifumo yako mbalimbali ya mwilini.
*Nasisitiza tena, chakula bora ni dawa*. *Tumia chakula kama dawa ili usije tumia dawa kama chakula.*
Jali sana kile ulacho na jithamini.
Maji ni uhai, pendelea kunywa maji mengi pia kila siku.
0 Maoni