FAHAMU KAULI 7 USIZOTAKIWA KUZIONGEA KWA MTEJA WAKO

 𝖪𝖠𝖴𝖫𝖨 𝖲𝖠𝖡𝖠 𝖹𝖠 𝖪𝖴𝖤𝖯𝖴𝖪𝖠 𝖪𝖴𝖹𝖨𝖲𝖤𝖬𝖠 𝖪𝖶𝖠 𝖶𝖠𝖳𝖤𝖩𝖠 𝖶𝖠𝖪𝖮 𝖨𝖶𝖤 𝖪𝖶𝖤𝖭𝖸𝖤 𝖲𝖨𝖬𝖴 𝖠𝖴 𝖠𝖭𝖠 𝖪𝖶𝖠 𝖠𝖭𝖠? 

.

1. HATA SIELEWI. ❌ (Jitambue vyema)

Badala yake Sema hivi, Hebu tuone Kama naweza kukusaidia Au Tatizo/Shida yako itapatiwa ufumbuzi subiri kidogo. ✓✓.

...

✳️Acha kumfanya mteja apigwe na butwaa kwa Kukuona hauna maana mbali na kumaini kwamba Unaweza kumsadia.Mpaka Mteja anaamua kukufuata wewe maana yake ni kwamba ameona wewe una utaalamu katika nyanja hiyo kwahiyo Onyesha Uwezo wako kwa kumpatia taarifa au maelezo yanayojitosheleza.


2. HAMNA SHIDA.❌  (Usimpe Uhakika)

Badala yake Sema hivi, Pole Sana unataka nikusaidiaje Au Nitazingatia ondoa Shaka ✓✓.

....

✳️Usikubali kirahisi (wewe) Funga mdomo wako na fikiria kwanza kabla ya kusema neno lolote kutoka katika kinywa chako kwasababu mteja huwa anapenda Uhakika wa Huduma Sasa Unaposema hamna shida ? Je ikitokea shida utafanya Nini (Sasa) hapo? Chunga Kauli zako.


.

3. HATUNA (SINA) CHA KUKUSAIDIA.❌

Badala yake Sema hivi,Ni kweli nilitamani kukusaidia Ila itakuwa ngumu Pole sana Au Unaweza ukajaribu (xxxx) pengine pale utapatiwa Msaada.✓✓.

....

✳️Usiseme Hatuna au hamna Cha kusaidia wakati ni WAJIBU wenu kuhakikisha kwamba wateja wanapata huduma sahihi au majibu ya matatizo Yao. Wateja huwa wananunua Tiba ya maumivu Yao kwahiyo hawezi MTU akanunua Simu kwako halafu ikamzimia akarudisha Ofisini kwenu mkasema Hamna Cha kumsaidia lazima ajiskie vibaya na ni WAJIBU wenu kumsaidia kwa namna yeyote ile.


4. HAIWEZEKANI .❌ (Onyesha Mbadala)

Badala yake Sema hivi, Mimi nitashindwa au Siwezi Ila wapo wanaoweza Kufanya au kukusaidia Au Itashangaza Sana Jambo Kama hili kushindwa kupatiwa ufumbuzi.✓✓

....

✳️Si sahihi kusema haiwezekani Sema Siwezi au Mimi nitashindwa kukusaidia kwasababu wapo wengi wanaoweza Kufanya Mambo magumu usiyoweza Kufanya badilika.


5. SINA UHAKIKA.❌ (Ijue Biashara yako)

Badala yake Sema hivi; Nalifahamu hili suala japo wapo wanaoshughulika nalo Au Nadhani jaribu Kufanya kwa njia (hii) nyingine.....✓✓

...

✳️Unaposema huna Uhakika maana yake ni kwamba  hauijui vyema biashara yako au huna Ratiba maalumu ya huduma yako kwahiyo unapaswa kuwa na Uhakika wa huduma unayoitoa au kuwa na Mtandao mkubwa wa watoa huduma wenzako ili wakusaidie kupata taarifa za kutosha.


6. HAPANA.❌ (Acha majibu ya Mkato) 

Badala yake Sema hivi, Mimi sihusiki Ila ngoja nikukabidhi kwa wanaohusika Au Unaweza ukajaribu sehemu nyingine.✓✓

...

✳️Ni kosa kubwa Sana kwa mtoa huduma  kumjibu mteja jibu la (Hapana) hata Kama hautoi huduma hii au Hauwezi kumsaidia kwani inakera Sana Ni heri usema Hapana.. Kwasababu kuliko Hapana Tupu. Usijifanye Umefika au Unajua Sana Utakula Jeuri Yao.


7. NDIYO...LAKINI.❌ (Acha Kuogopa)

Badala yake Sema hivi, Ndiyo nitakupatia mrejesho Kamili Au Ndiyo Nimekuelewa ngoja nifuatilie Kisha nitakurejea punde.✓✓

...

✳️Usitoe majibu ya "Ndiyo...lakini" kwasababu yanaonyesha wasiwasi au Hali ya kutokuwa na Uhakika wa hicho unachotaka kukisema.


8. NITAKUTAFUTA BAADAE KIDOGO.❌

Badala yake Sema hivi, Nimekuelewa ngoja nitafute majibu halafu nitakupigia au Nitakutaarifu nikupe mrejesho Kamili Au Nakuthamini Sana Ila namalizia Kumhudumia mteja Mara moja nitakupigia Mimi muda siyo mrefu.✓.

...

✳️Ukipigiwa Simu na mteja usiikate hata Kama upo busy  ni heri uache iite na Ukipokea usimwambie tu nitakupigia Baadae Bali msikilize kidogo Kisha tumia kauli hizo Hapo juu au Kama Sivyo andika Ujumbe wa Kumwomba akuvumilie kidogo labda upo kikaoni n.k.


9. KUMUULIZA JINA LAKE TENA (X 2).❌

Badala yake Sema hivi , Nimekusikiliza kwa Makini Sana Kuanzia Mwanzo mpaka mwisho ulisema Nani Kweli ?? Au Sasa Naomba Majina yako kamili matatu niyahifadhi kikamilifu sasa✓✓ 

....

✳️Kitendo Cha Kumuuliza mteja Jina lake mara ya Pili (2) wakati mwanzoni alikwisha kuambia, Hiyo ni kero kubwa kwasababu unaonyesha jinsi gani hukuwa makini wakati anazungumza na wewe (maana yake Haujali)

.

.

.

.

Badilisha Kauli zako kwani Mdomo wako ndiyo unakuponza Bila hivyo utapoteza au utashindwa kupata wateja wengi zaidi.

Chapisha Maoni

0 Maoni