SULUHISHO LA MVURUGIKO WA HOMONI SASA LAPATIKANA.

 *SOMO FUPI LA UELEWA KWA WANAWAKE, KUHUSU HORMONES*


• Kwa nini Homoni Zetu Huvurugika..!


>>Homoni zipi zenye athari  zaidi...?


*Kwani HOMONI NI NINI?*

======>Homoni ni kichocheo ambacho hutengenezwa na tezi mbalimbali mwilini. Na homoni husafirishwa na damu kwenda sehemu inapohitajika mwilini.


 Kila homoni huwa ina kazi yake maalumu, huwezi kukuta homoni ya uzazi inaenda kuchochea umeng’enyaji wa chakula cha protini.


 Kila homoni na kazi yake maalumu.


Homoni kwa tafsiri nyingine tunaita ni “Kichocheo” kwa sababu madhumuni ya kutengenezwa kwa homoni ni kwenda kuchochea tendo fulani la kibaolojia litokee mwilini.


Mfano: Homoni ya kike estrogen hutengenezwa na tezi iitwayo ovari na huenda kuchochea mambo mbalimbali kwa mwanamke kama kubarehe kwa mwanamke (Kuota matiti, Ngozi laini, nyoga kuongezeka, sauti nyororo), pia huchochea kujengeka kwa ukuta wa kizazi ili mimba ije ishike kwenye ukuta imara. Kwa maana hiyo homoni ni “Kichocheo cha mwili”.


Homoni zipo aina nyingi, kuna homoni za uzazi, usagaji chakula, zinazo ratibu matumizi ya wanga, mafuta na protein n.k ila katika somo hili utajifunza homoni za uzazi kwa mwanamke.


Homoni ambazo zinachochea matukio mbalimbali ya uzazi kwa mwanamke ni Estogen, Progesterone, Prolactin, Follicle stimulating hormone(FSH), Luteinizing hormone (LH), na Testosterone.


Homoni hizi huwa zinatengenezwa na ovari kwa mwanamke lakini tezi inayoratibu kiwango cha usawa wa homoni hizi ili isije ikatokea moja ikapanda sana na nyingine ikashuka sana. Kazi hiyo hufanywa na tezi iliyopo kwenye ubongo iitwayo Anterior Pituitary Gland.


 Kwa hiyo tezi hii ina hakikisha kwamba hakuna homoni inayozidi wala inayopungua.


Kazi za homoni hizi:


•Estrogen

>Huchochea matendo yote wakati ya kubalehe. Kuota matiti, Ngozi kuwa laini, sauti, nyonga kuongezeka n.k

>Hujenga ukuta wa kizazi ili mimba ijishikize kwenye ukuta mnene.

>Huchochea ukuaji wa matiti wakati una mimba.


•Progesterone

>Hutengenezwa na tezi ya dharura (corpus luteum) pale ambapo yai limetoka

>Kazi yake kubwa ni kulea mimba, inaongezeka sana baada ya siku ya kupevuka kwa yai na baada ya mimba kutungwa.

>Endapo mimba isipotungwa homoni hii inayoshikilia ukuta usibomoke hushuka kiwango chake na ndipo inawezesha ukuta kuporomoka kwa kutoa uchafu (damu ya hedhi) ili kwamba ukuta mwingine ujengwe kwa mzunguko ujao

>Pia hukuza matiti wakati una mimba na kuendelea kufanya ukuta wa kizazi uwe imara sana

 

•Prolactin

>Hii ni homoni ambayo hupanda sana wakati una mimba na unakaribia kujifungua

>Hutengeneza maziwa yakutosha ili uweze kunyonyesha

>Huwa ina mkinga mama asipate mimba mapema akiwa ananyonyesha. >Ukiwa unanyonyesha homoni hii huwa nyingi na huzuia upevushaji wa mayai. Ila unashauriwa baada ya wiki sita tangu umejifungua kuwa makini maana kwa unyonyeshaji wa nadra kwa wanawake wengi unasababsha prolactin kutokuwa katika kiwango toshelevu kuzuia upevushaji wa mayai.


•Testosterone

Tunaita hii ni “homoni ya kiume” kwa sababu huwa ndio imetawala (inajionesha kuwa juu) kwa mwanaume kuliko homoni zingine. Lakini wanawake pia huwa wana hii homoni katika kiwango kidogo sana. Wao homoni inayotawala ni estrogen.

>Homoni hii inasaidia sana uhifadhi wa mafuta mwilini, pia inasaidia katika utumiaji wa vyakula vya mafuta,protini na wanga, pia inasaidia sana kutengeneza misuli ya mwili wako. Hivyo ni ya muhimu sana kwa mwanamke.

 

•Follicle Stimulating Hormone (FSH)

>Hii ni homoni ambayo inakomaza mayai, na huanza kupanda kwenye damu siku ya kwanza tu umeanza kuingia hedhi. >Yenyewe inaanza kuandaa yai ambalo litapevuka siku ya 14 katika mzunguko wako.


•Luteinizing hormone (LH)

Ni homoni ambayo husaidia yai liweze kutoka kwenye kiwanda yaani ovari na ndipo lije kwenye mirija ya uzazi kwa ajili ya urutubishaji.


Mambo ya Kuzingatia juu ya umuhimu wa homoni hizi

 


Homoni hizo zote kwa mwanamke hutengenezwa na ovari na malighafi ya utengenezaji ni kiini lishe kiitwacho cholesterol au lehemu.

Homoni zote hizo kiwango chake huratibiwa na tezi iitwayo Pituitary gland, na njia nyingine za kudhibiti homoni moja isipande sana huwa tunaita “Negative feedback inhibition” yaani pale ambapo homoni moja imeongezeka au inajitosheleza taarifa inapelekwa kwenye ubongo (pituitary) ili isitengeneze au itengeneze kidogo. Njia hii ndio wanasayansi walitumia kuweza kutengeneza vidonge, sindano na pandikizi za uzazi wa mpango. Hizo ni homoni ambazo zinaenda kuzuia tezi ya pituitary isitengeneze homoni zinazokomaza mayai na kupevusha mayai yaani FSH na LH hazitatengenezwa.

 


*Je nitajuaje homoni zangu zipo vizuri?*


Kuna kipimo cha maabara unachokuliwa sampuli ya damu na mtalamu wa maabara ataenda kufanyia kazi damu yako na kukuletea majibu baada ya siku moja mpaka mbili unaweza pata majibu.


Homoni za mwanamke huwa zinapanda sana kuanzia muda wa kubalehe na zinaanza kushuka pale unapoelekea kwenye kikomo cha hedhi miaka 50.

*•Kuvurugika kwa homoni(HORMONES IMBALANCE) maana yake ni nini?*

====>Maana yake ni kwamba homoni zako haziko katika mhimili unaotakiwa na zinasababisha kwa namna moja au nyingine mzunguko wako wa hedhi unakuwa sio salama na linaweza kusababisha kutobeba hata mimba, inategemea na ukubwa wa tatizo lako.


Tazama mifano hii hapa chini 👇👇👇


Endapo homoni ya estrogen ikiwa juu sana inaweza kukuhatarisha ukapata magonjwa yafuatayo;

i./ Shinikizo la damu

Hii ni kwa sababu homoni ya estrogen huenda kuishinikiza figo kuzuia madini ya chumvi (sodium) yasitoke nje. Na kadri unavyozuia madini haya ya chumvi yasitoke huenda sambamba na kuzuia maji. Hivyo hii inaweza kupandisha kiwango cha damu (plasma) na kusababisha Shinikizo la damu, moyo kupanuka, kuvimba miguu n.k


ii./ Kansa na uvimbe kwenye kizazi (fibroids)

Homoni hii ikizidi mwilini huenda kuchochea seli za titi, ukuta wa kizazi kukua kwa kasi sana na zinaweza kuchochewa na kubadilika kuwa kansa. Hivyo homoni nyingi ya estrogen inakuweka hatarini kupata kansa ya titi (breast cancer), kansa ya kizazi (Endometrial cancer) na baadhi ya kansa za Ubongo.


•Homoni ya progesterone inapokuwa chini sana inaweza kusababisha yafuatayo

>Kuwa na maumivu makali sana ya hedhi

>Kuingia hedhi yenye kuambatana na kutokwa na damu nyingi sana na kwa muda mrefu

>Mimba kuwa zinatoka, kila unapobeba mimba inatoka hata kabla haijamaliza miezi 3.


•Homoni ya Prolactin ikiwa juu sana kwenye damu unaweza kupata matatizo yafuatayo kiafya

Kumbuka homoni hii inapanda unapokuwa una mimba na unanyonyesha tu. Lakini ukikuta ipo juu sana kwenye damu wakati hunyonyeshi na huna mimba kiafya inakuwa sio salama.

>>Inaweza kusababisha kutokwa na maziwa wakati huna mimba na hunyonyeshi. Chuchu zikawa zinatoa maziwa.

>Huwezi kubeba mimba kabisa kwa sababu prolactin ikiwa juu wakati huna mimba huenda kuzuia ovari zisikomaze na zisipevushe mayai kabisa. >Unakuwa unaingia hedhi ambayo hairutubiki.

>Matiti kuwa yanajaa na kuuma sana hasa unapokaribia hedhi


•Homoni ya testosterone ikiwa juu kwa mwanamke unaweza kupata madhara yafuatayo kiafya;

>Kutokuwa unapevusha mayai hata kidogo hii inaweza kusababisha ukawa mgumba.

>Mayai yanakuwa hayapevuki na matokeo yake unapata aina ya uvimbe kwenye ovari tunaita “Cysts”. Ambapo cyst inaweza kuwa moja na kubwa au zinaweza kuwa nyingi “Polycysts”. Kwa hiyo unakuwa hatarini kupata uvimbe kwenye ovari.

>Kuota nywele sehemu ambazo mwanamke hutakiwi kuwa na nywele. Mfano ndevu kwa mwanamke, nywele kifuani n.k

>Hamu ya tendo la ndoa hupotea kwako inakuwa ni maumivu tu wakati wa tendo la ndoa.


Mara nyingi mvurugiko wa hormones wa muda mrefu husababishwa na ulaji wetu usiofaa na matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango


*Dalili ambazo mara nyingi hujitokeza kuashiria kuwa hormones zako haziko sawa ni pamoja na*


>>Ukavu ukeni

- Maumivu wakati wa tendo la ndoa

- Kutoa jasho jingi usiku

- Maumivu chini ya kitovu  wakati wa hedhi

- Upungufu wa hamu ya tendo la ndoa

- Mabadiliko ya siku za hedhi na kupata hedhi kwa muda mrefu unaozidi siku Saba

-Kukosa ute wa uzazi

-(heavy bleeding, au kujaza pedi moja kwa saa moja)

- Kukosa hedhi kwa muda mrefu, na kutoa damu yenye mabonge mabonge wakati wa hedhi

- Uchovu wa mara kwa mara bila sababu

- Hasira za mara kwa mara

- Kukosa usingizi


Njia sahihi ya kuliepuka hili ni pamoja na kujiwekea utaratibu wa kula, mboga za majani, supu ya nyama au mchemsho wa ndizi, kitunguu maji, korosho, viazi vyekundu, fenesi, mrehani, asali mbichi, maziwa aina yoyote, msamitu, soya, mbegu za tikiti au maboga, mapera, mimea jamii ya mikunde, tende na karoti huku ukiachana na soda, vinywaji baridi wakati wa hedhi, kahawa na ngano ya kukobolewa kama mkate mweupe, chapati na maandazi...


Kama una dalili zaidi ya moja kwa mfano tuseme huwa unahisi maumivu ya kiuno, uchafu kutoka ukeni, mgongo kuuma, maumivu chini ya kitovu, kuhisi hali ya homa baadhi ya nyakati, kukosa hamu ya kufanya mapenzi, kuwa mkavu wakati wa kufanya mapenzi na dalili nyinginezo kuhusiana na mfumo wa uzazi hapo ninakushauri kuchukua dawa hizi tano (5) na kuanza kuzitumia Mara moja iwezekanavyo

*Femicare*

*Reish coffee*

*Refined yunzhl essence*

*Pure and broken*

*Zaminocal Cap's*


Kama tatizo limeshakuwa sugu kiasi limepelekea  kushindwa kunasa na unahitaji mtoto kwa haraka ili kuleta amani ya moyo na hata ndani ya ndoa, ninazo dawa za asili na si chemical kwa ajili ya kusafisha mirija, kuondoa uchafu katika uzazi na kuongeza wingi wa homoni ili mzunguko wa hedhi uzidi kubalansi + mayai kupevuka kwa wakati na kulea mimba isichoropoke.


 *Nicheki faster in-box kwa namba zangu hizo* *0719197319*

*0763132806*

Chapisha Maoni

0 Maoni