Bila Shaka. unataka kujua jinsi ya kupanga malengo yako kwa Usahihi? (si NDIYO )???. . . Hivi Umewahi kujiuliza ni furaha ya jinsi gani au kiasi gani anayoipata mtu pale anapofanikiwa kutimiza malengo yake.?.........mmmmmmh Sijui....(🤷) . labda nikuulize swali moja lakini naomba pia uwe muwazi katika hili," hivi Mara ya mwisho kupanga malengo (yaliyoandikwa) ilikuwa ni lini? na yalikuwa yanahusu Nini?" Mimi sijui unawaza nini hivi Sasa hebu jipe majibu mwenyewe Kisha tafakari wapi ulikosea. . Nina habari njema kwako kwani nimekuwa nikifanya tafiti mbalimbali ili kubaini Tatizo lipo wapi na Ufumbuzi umepatikana kwa ajili yako wewe unayesoma Ujumbe huu.Je ! Unajua kwamba ni Asilimia 5% tu ya watu huyaandika malengo Yao kwenye karatasi au notebook? (Unadhani wewe upo kwenye kundi lipi Kati ya asilimia 5% au 95% iliyobakia ?).... . Ahahaha! Sasa Wala Usijali Tena kwani Tatizo lako limepatiwa Ufumbuzi tayari ondoa Shaka. . Nisikilize nikuambie rafiki yangu ili uweze kupanga malengo yanayofika Basi ni lazima upitie hatua hizi kumi (10) kwanza kwani bila hivyo utashindwa kufanikiwa na watu wengi wamekuwa wakishindwa hapa (tu). Najua Kuna mfumo Fulani umeuzoea na unauamini (sana) na tena unahisi bila Huo Hauwezi kufanikiwa! (SI NDIYO,?) Usijali nataka tu nikuhakikishie kwamba endapo Kama utafuata hatua hizi zilizoanishwa hapo chini Basi ni dhahiri kabisa 100% ya malengo uliyonayo yatakwenda kutimizwa. . Ina maana mwisho wa kila Wiki, Mwezi ,au mwaka wewe utakuwa ni mtu wa kuchekelea....tu (ahahaha) ndiyo hivyo bwana Mwako wako huu Sasa hebu.......... . . Twende ukazione hatua hizo 10 (sahihi) 🌀1. Ainisha malengo yako yote. (Afya,Elimu ,Uchumi, Mahusiano n.k ,Ipo hivi chochote unachokiona nimefanikiwa kwa viwango vya juu basi jua wazi kilipangwa na kilianza Kama Wazo mwanzoni) . 🌀2. Yaandike Malengo kwenye notebook. (Ipo Nguvu katika kuandika malengo yako kwani Hiyo ndiyo hatua ya awali ya kugeuza mawazo kuwa Halisi. 🌀3. Yachambue Malengo yako. ( Hakikisha unatofautisha Kati ya malengo endelevu na malengo ya muda mfupi ili Kusudi unapokuwa unataka kupanga mikakati ujue wazi wapi unapaswa kuiwekeza Nguvu zako zote kulingana na Muda ulionao, weka vipaumbele kwenye Mambo ya Muhimu kwanza) 🌀4. Ainisha Faida na Changamoto. Ni kweli unataka kufanikiwa Ila Ni lazima pia uainishe baadhi ya Mambo ambayo unahisi yatakuwa kikwazo kwako na baada ya Kufanya hivyo Hakikisha unakuja na mkakati maalumu kwa ajili ya kukiondoa au kukishinda kikwazo au vikwazo husika. Mfano Unataka kwenda Jeshini Kufanya Kazi lakini unajua kabisa Jeshini huwezi kupata muda kirahisi au Umeomba Kazi ya Utabibu (uDaktari) kwahiyo ukiipata unajua kabisa kwamba Kuna muda utahitajika kukatisha usingizi wako uende kuokoa Maisha ya watu ,Mfano mwingine Labda wewe ni Mlinzi unayatoa Maisha yako kushinda njee usiku Kucha kupigwa na baridi na hatari kadha wa kadha kwahiyo ili uwe Salama huna budi kununua makoti mazito pamoja na Silaha. 🌀5. Orodhesha Nia (Kusudi la lengo husika) Mfano: 1.Kujenga nyumba ili nipunguze kulipa Kodi. 2. Kufanya mazoezi ili nipunguze unene. 3. Kupata leseni ili ninunue gari. 🌀6. Tengeneza Mkakati Bora (Action plan) Malengo bila utekelezaji sawa na bure kabisa hivyo Hakikisha unayasimamia na kutenda kwa kuweka mkakati aidha wa Wiki,Mwezi,Miezi,Mwaka,Miaka. Mfano kila wiki lazima niweke akiba ya Tshs 20,000/-.(Lengo la Kifedha) 🌀7. Washirikishe Watu sahihi. Ili uweze kupata Nguvu ya kuyatekeleza malengo yako basi huna budi kuwashirikisha watu sahihi Mfano! Marafiki ,wazazi n.k Ukweli ni kwamba hata wazazi wako au Marafiki wanaweza wasikuunge mkono kabisa kulingana na uhaba wa Imani walionao kwahiyo Wala Usiogope Wewe simamia malengo yako. Ukiwaambia watu kuhusu malengo yako utapata msukumo wa ndani wa kuyakamilisha ili mwisho wa siku usiwape na nafasi ya kukuuliza (mbona haufanyi) . 🌀8.Ufuatiliaji wa kila Mara . Naomba nikupe Mfano mdogo Chukulia ukiwa unachemsha Maziwa jikoni si lazima ukae unayakodolea macho ili Kusudi yasimwagikie?? eeeh au pengine ukiwa unapika wali lazima uwe Karibu kuepuka kuunguza Si NDIYO! ..Vivyo hivyo kwenye upande wa malengo pia huna budi kuyasimamia ili mwisho wa siku uyatimize na unachopaswa kujua Ni kwamba haya malengo Ni kwa ajili yako wewe mwenyewe kwahiyo hakuna mtu wa kuyasimamia vyema usipokuwa wewe mwenyewe. 🌀9. Furahia na Jipongeze kila hatua . Hakuna mtu atayeijua furaha yako halisi uliyonayo pale utakapokamilisha Mambo uliyoyapanga Kwahiyo Hakikisha unafurahia hatua ndogo ndogo kila siku kwenye maisha yako usisubirie watu wakwambie hongera wewe Jipongeze mwenyewe (NO ONE IS COMING) kila MTU yupo busy na Mambo yake. . 🌀10. Yafanyie tathmini malengo yako inaweza kuwa ni kila baada ya wiki moja Kama Ni malengo ya Mwezi mmoja au kila baada ya mwaka mmoja Kama malengo yako Ni miaka 5-10 ijayo. Kwahiyo Hakikisha unafanya MABORESHO katika mbinu na mikakati ya namna Bora katika utekelezaji wa malengo yako. . . NYONGEZA ! .(SIFA ZA MALENGO SAHIHI) ✳️1.Upekee (Specific) Hakikisha unachagua malengo Maalum (upekee) kwa ajili yako kwa Mfano:1 badala ya kusema mwaka 2021 nataka niwe na Pesa nyingi kwenye akaunti yangu , weka wazi ni kiasi gani labda million 100,000,000/- Au Million 3,000,000/- .Mfano:2 Badala ya kusema tu nataka nianze kwenda Gym (mazoezi) weka lengo kabisa kwa usahihi (upekee) unakwenda gym KUPUNGUA au kujaza Mwili.. ✳️2.Yanayopimika (Measurable) Siri ya Ushindi imejificha katika kuyapima malengo yako.Hebu Jiulize hivi kwa wewe jinsi unavyojiona na Hali yako ilivyo Sasa utaweza kweli kununua gari?? Au kwa namna ambavyo mwenendo wa majukumu yalivyoongezeka utaweza kweli Kutunza kiasi kikubwa Cha Pesa Benki ?? au Utaweza kweli kuoa au kuolewa kulingana na Tabia uliyonayo? ✳️3.Yanayofikika (Achievable). Panga malengo yanayofikika Hauwezi kupanga kwenda nchi za nje ilihali hujui unataka kwenda nchi gani ? kwanza ainisha nchi unayotaka kwenda katengeneze passport Kisha Fuatilia lengo lako. Hauwezi kupanga kununua gariwakati kuendesha tu haujui na istoshe hata leseni huna ! kwahiyo tafuta kwanza leseni Jifunze kuendesha Kisha Nunua gari. ✳️5.Yenye Uhalisia (Realistic) Ni ngumu Sana kupanga malengo yasiyo na uhalisia kwa Mfano unasema mwaka 2021 nataka nijenge nyumba ANGANI inayoelea??. Ni Jambo zuri kuwa na fikra dhahania lakini unachopaswa kujua kwamba Kuna baadhi ya Mambo mengine hayawezekaniki kutimizwa. panga malengo yaliyo ndani ya uwezo wako huwezi kusema kwamba Unataka ugombee kiti Cha urais wakati una miaka 18 hahahaha... ✳️6.Ukomo/Mipaka (Deadline) Ili uweze kuyatimiza malengo yako kulingana na Muda rasmi au Ratiba maalumu Basi huna budi kuwa na UKOMO AU DEADLINE yaani kwa Lugha rahisi Ni hitimisho. Kwa Mfano Unaweza ukaweka lengo la muda na a kudumu kila siku kwamba ukizidi saa mbili na nusu za Usiku Basi huli Chakula. . . . Bila shaka umejifunza Mambo ya msingi Sana kuhusu hatua pamoja na sifa za malengo yanayofikika , kwahiyo ushindwe tu wewe kutimizwa ndoto zako Mimi Sina mengi nikutakie siku njema Mungu akubariki. . . Ila Kama Wewe unahisi Hauwezi kujisimamia mwenyewe Basi kwa gharama nafuu Sana Utasimamiwa vyema na Mimi (Mentoring). Nipigie/nitext/ Niambie/Nitafute/Nikusaidie. 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇 . . Mr.Kalungu psychomotive P𝐬𝐲𝐜𝐡𝐨𝐥𝐨𝐠𝐢𝐬𝐭|Counsellor|Trainer
0 Maoni