![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUawLVrhh8ri6HbBhupb_4Xa1_K3uTejj36LpJJcKOQlcm8F8xbjgplQE41Wnv6c-RZnj3YGmNpTlPVO2TODRM8a-EJmxjPsU3o9y9U2mfmk14zXvY6fJPvCWymWum3FMoUSCQqlWXcoyG/s320/IMG-20201126-WA0012.jpg)
Saratani ya matiti (breast cancer) ni kansa inayotokea kwenye tishu za matiti. Inatokea kwa wanaume na wanawake. Saratani ya matiti kwa wanaume hutokea kwa nadra. Dalili za saratani ya matiti ni pamoja na; Kuvimba titi, kuchubuka au kubonyea kwa ngozi ya titi, maumivu ya titi/chuchu, kurudi ndani kwa chuchu (retraction), wekundu, kukakamaa kwa ngozi ya titi na kutokwa na majimaji kwenye matiti (tofauti na maziwa). Matibabu hujumuisha upasuaji, tiba ya mionzi, tibakemikali, tiba ya homoni na tiba za kulenga seli za kansa (targeted therapy). WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA SARATANI YA MATITI Umri: Hatari ya kupata saratani ya matiti huongezeka kadri umri unavyoongezeka. Wengi ni miaka 60 kuendelea. Historia binafsi ya kuwa na saratani ya matiti: Mwanamke aliyekuwa na saratani katika titi lake moja, ana hatari kubwa ya kupata kansa katika titi lake jingine. Historia ya uzazi na hedhi: Kadri mwanamke anavyochelewa kupata mtoto wa kwanza ,ndivyo na hatari yake ya kupata saratani ya matiti inavyoongezeka. •Tiba ya mionzi kifuani: Wanawake ambao walipata tiba ya mionzi kwenye kifua kabla ya umri wa miaka 30 wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya matiti. •Unene au kitambi baada ya damu ya hedhi kukata,Ukosefu wa mazoezi,Unywaji wa pombe n.k....tutaendelea...! MAMBO YA KUFANYA KUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA SARATANI YA MATITI 1•Mazoezi: Kufanya mazoezi kwa angalau masaa 4 kwa wiki kunasaidia kupunguza homoni mwilini na kupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti 2•estrojeni: Kupungua kiwango cha homoni ya estrogen mwilini husaidia kuzuia saratani ya matiti. Hali zifuatazo zinapunguza homoni ya estrojeni mwilini: 📍Mimba: Viwango vya estrojeni hupungua wakati wa ujauzito. Hatari ya kupata saratani ya matiti inaweza kupungua zaidi kwa wananwake waliozaa mtoto wa kwanza kabla ya umri wa miaka 20. Kunyonyesha: Viwango vya estrogen hubaki chini wakati mwanamke anaponyesha. 📍Kuondoa ovari: Ovari hutengeneza estrojeni. Kuondoa ovari moja au zote mbili hupunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha estrojeni. Pia, kuna madawa yanaweza kupunguza kiwango cha estrojeni kinachotengenezwa na ovari. 📍Kuchelewa kuvunja ungo: Kuanza kupata hedhi katika umri wa miaka 14 au zaidi kunapunguza uwezekano wa kupata kansa ya matiti. 📍Damu ya hedhi kuwahi kukata: Mwanamke anapopata hedhi kwa miaka michache tu, uwezekano wa kupata saratani ya matiti hupungua. Hedhi inapokatika mapema (early menopause) estrojeni hupungua pia. USISITE KUWASILIANA NAMI KWA MSAADA NA USHAURI JUU YA TATIZO LOLOTE KIAFYA
0 Maoni