*USISOME KAMA HUTAKI MABADILIKO KWENYE MAISHA YAKO*

Ni kweli unatamani mabadiliko kwenye maisha yako lakini hujui kwanini mabadiliko kwako ni kitendawili kikubwa ambacho unashindwa kujua kutegua kujua wapi unapokwama na kushindwa kupata mabadiliko unayo yataka kwenye maisha yako  »»» Unapaswa kujua unataka mabadiliko kwa kutaka kubadilisha jana yako na mambo yaliyopita, sababu hakuna anayeweza kubadilisha jana yake ngumu kupata mabadiliko kama kila siku unaishi kwa kufikiria kwa mambo yaliyopita   Sababu unapofikiria mambo yaliyopita huwezi kubadilisha makosa yako uliyofanya, na makosa uliyofanya yanageuka majuto na ndio msemo wa wahenga "Ningelijua nisingefanya" na majuto yanatesa sana   "No man is rich enough to buy his past"  (Hakuna mtu yeyote ambaye ana utajiri wa kuweza kununua mambo yaliyopita)- Oscar Walde  Acha kufikiria kubadilisha jana yako maana jana yako ndio inakuzuia wewe kuweza kufanya mambo makubwa leo yenye kujenga kesho bora  Badilisha mtazamo wako wa kuamini maisha yako yanajengwa na mambo yaliyopita, anza sasa kuishi kwa kuamini leo ndio siku muhimu kukamilisha ili ubadilishe kesho yako    "You can not change your past, but you can change your future by action of today"  (Huwezi kubadilisha mambo yaliyopita lakini unaweza kubadilisha mambo yajao kwa hatua unazochukua leo)  »»» Mabadiliko ni kuanza kuchukua hatua kuanza leo na sio kughairisha kila siku kusema utafanya lakini  hakuna hatua ambazo unachukua ili kubadilisha historia ya maisha yako leo ili kesho yako iwe bora kuliko leo, anza kufanya leo kwa kuacha kughairisha kila siku  »»» Siri usiyoijua ni kwamba msingi wa mabadiliko ni maamuzi wa kutaka mabadiliko na sio kujenga matamanio ya kutaka kubadilika lakini hakuna maamuzi uliyochukua ili upate mabadiliko chanya  Kuwa miongoni mwa watu wachache waliopata mabadiliko muhimu kwenye maisha kwa kuchukua maamuzi ya kijasiri kwa kufanya  Mabadiliko yanawafikia wote wenye kuchukua maamuzi yenye kujenga kesho yao iliyo bora  »»»» Ndio unataka mabadiliko huna budi kuanza kuambatana na watu wenye kupenda mabadiliko kwenye maisha yao, watu unaombatana nao ndio wamebeba ushindi au kufeli kwako katika mabadiliko unayotamani kuyapata    *Ni bora uwe pekee yako kuliko kuambatana na watu ambao sio sahihi kwenye maisha yako*   Kasi ya mabadiliko kwenye maisha yako inabebwa sana na watu ambao muda mwingi unakuwa nao, kuwa makini  »»»» Mabadiliko ni kuchukua hatua kwa vitendo baada ya kujua maamuzi gani uchukue ili mabadiliko unayotaka yaweze kuleta matokeo, acha kuleta visingizo ya kwanni umeshindwa kupata mabadiliko uliyotamani kuyapata  »»»» Unatamani kupata mabadiliko kwenye eneo lipi kwenye maisha yako?  _______ Kauli Mbiu: "MAISHA  NI KUTHUBUTU"  Imeandikwa:  Innocent Ngaoh (Life Coach, Author & Inspirational Speaker)  ________ Email: Innocentabisai98@gmail.com  Instagram & Facebook: Lolo_facts

Chapisha Maoni

0 Maoni